Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb19 Oktoba uku. 8
  • Yehova Anawapenda Watu Safi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova Anawapenda Watu Safi
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2019
  • Habari Zinazolingana
  • Usafi Unamaanisha Nini Hasa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Usafi Ni Muhimu Kadiri Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Mungu Anawapenda Watu Walio Safi
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
  • Usafi—Kwa Nini Ni Muhimu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2019
mwb19 Oktoba uku. 8
Ndugu akisafisha choo kwenye Jumba la Ufalme

MAISHA YA MKRISTO

Yehova Anawapenda Watu Safi

“Nawa mikono. Safisha chumba chako. Fagia sakafu. Nenda utupe takataka.” Wazazi wengi huwafundisha watoto wao jinsi ya kudumisha usafi wa kimwili. Hata hivyo, Mungu wetu mtakatifu ndiye chanzo cha usafi. (Kut 30:18-20; Kum 23:14; 2Ko 7:1) Tunapodumisha miili yetu na vitu vyetu vikiwa safi, tunamletea Yehova heshima. (1Pe 1:14-16) Namna gani kuhusu nyumba zetu na mazingira yetu? Tofauti na watu wanaotupa takatakata barabarani na kwenye bustani, Wakristo hujitahidi kuidumisha dunia ikiwa safi. (Zab 115:16; Ufu 11:18) Hata mambo madogo, kama vile kutupa karatasi za peremende, chupa za maji na soda, au big-G (chingamu), kunaweza kufunua mtazamo wetu kuhusu usafi. Katika maisha yetu yote, tungependa “kujipendekeza kuwa wahudumu wa Mungu.”—2Ko 6:3, 4.

TAZAMENI VIDEO MUNGU ANAWAPENDA WATU WALIO SAFI, KISHA MJIBU MASWALI YAFUATAYO:

  • Huenda watu wakatoa visingizio gani vya kutodumisha vitu vyao vikiwa safi?

  • Sheria ya Musa ilifunuaje maoni ya Yehova kuhusu usafi?

  • Tunawezaje kutoa ushahidi kimyakimya kumhusu Yehova?

Baba akiingia kwenye gari chafu la mwana wake; baba na mwana wakizungumzia viwango vya Yehova vya usafi; makuhani wawili katika Israeli la kale wakiwa kando ya beseni la kunawia la shaba; kikundi cha utumishi wa shambani kikitoka katika gari safi la yule kijana

Ninawezaje kuonyesha mtazamo wa Yehova kuhusu usafi katika maisha yangu binafsi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki