Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w21 Februari uku. 25
  • Kwa Sababu tu ya Tabasamu!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Sababu tu ya Tabasamu!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2021
  • Habari Zinazolingana
  • Kumkumbuka Muumba Wetu Kutoka Ujanani Kuendelea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Kazi Nyingi za Akina Mama
    Amkeni!—2002
  • Manufaa ya Ulimwenguni Pote ya Kuhubiri kwa Kutumia Vigari
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Utafutaji Wangu Wenye Mafanikio wa Maana ya Uhai
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2021
w21 Februari uku. 25

Kwa Sababu tu ya Tabasamu!

Helen akitabasamu huku akiwa amesimama kando ya kigari cha machapisho. Wanawake wawili wanapita mbele yake.

WANAWAKE wawili vijana walikuwa wakitembea pamoja kwenye eneo la biashara katika jiji la Baguio, nchini Ufilipino. Walikiona kigari cha mahubiri ya hadharani, lakini hawakukisogelea. Helen, dada aliyekuwa amesimama kando ya kigari hicho, aliwaonyesha tabasamu kubwa. Wanawake hao waliendelea na safari yao, lakini walipendezwa na tabasamu yenye uchangamfu ya Helen.

Baadaye, wanawake hao walipokuwa wakirudi nyumbani wakiwa kwenye basi, waliona ubao mkubwa wenye ishara ya jw.org kwenye Jumba la Ufalme. Walikumbuka kwamba yalikuwa maandishi yaleyale yaliyokuwa kwenye kigari cha mahubiri ya hadharani. Wakashuka kwenye basi na kuangalia ratiba ya mikutano ya makutaniko mbalimbali yaliyoorodheshwa kwenye lango la Jumba la Ufalme.

Wale wanawake wawili wakitabasamu baada ya kumwona Helen kwenye Jumba la Ufalme.

Wanawake hao wawili walihudhuria mojawapo ya mikutano iliyofuata. Na ni nani waliyemwona walipoingia ndani ya Jumba la Ufalme? Helen! Walitambua mara moja kwamba yeye ndiye aliyewaonyesha tabasamu kubwa siku ile. Helen anasema, “Waliponifuata, nilipata wasiwasi kidogo. Nilifikiri labda nimefanya jambo fulani baya.” Lakini wanawake hao walimwambia Helen kilichokuwa kimetukia.

Wanawake hao vijana walifurahia mkutano na ushirika; walijihisi wakiwa nyumbani. Walipowaona wengine wakifanya usafi wa jumba baada ya mkutano, waliomba ikiwa wao pia wangeweza kusaidia. Mmoja kati ya wanawake hao aliondoka nchini, lakini mwingine anajifunza Biblia—kwa sababu tu ya tabasamu!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki