Matendo ya Mashahidi wa Yehova Katika Nyakati za Kisasa
Mtume Petro alishangaa. Tangu utoto yeye alikuwa amefundishwa kuepuka Mataifa wasiotahiriwa. Sasa, Mungu alikuwa akimwambia awatembelee na hata awe rafiki yao. Kwa hiyo kwa kutii Petro aliondoka mji wa bandarini wa Yofa na kusafiri kaskazini kwenye bandari ya Kaisaria. Huko yeye akaingia ndani ya nyumba ya Mtaifa mmoja—Kornelio. Ile sehemu inayobaki ya hadithi hiyo Mashahidi wa Yehova wote wanaijua sana. Kornelio na nyumba yake wakawa wa kwanza wa mstari mrefu wa waongofu wasio Wayahudi unaoongoza kwenye Ukristo.—Mdo. 10:1-48.
Kama Petro, Mashahidi wa Yehova leo wamekuwa na nia ya kueneza “zile habari njema” kila mahali na kwa kila mmoja, kama yanayofuata yaonyeshavyo.—Mdo 10:36.
AILANDI: Karibu miaka mia moja iliyopita, yule msimamizi wa kwanza wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi alisafiri kutoka United States akapanue kuhubiriwa kwa habari njema. Bandari yake ya kwanza aliyotembelea ilikuwa Ailandi. Ulikuwa mwaka 1891. Yeye aliripoti: ‘Ailandi ni shamba lililo tayari kuvunwa.’ Lakini watu wa Mungu wangepata mambo gani katika kupanda na kupalilia mbegu za Ufalme wakielekeana na migawanyiko, vitendo vya watu wenye ghasia, na uvamizi wenye kuogofya?
KOREA: Ule mwaka wa 1914 ulionyesha mwanzo wa kuchapishwa kwa ujumbe wa kweli wa Kikristo katika lugha ya Korea. Lakini si kila mmoja kule aliyethamini ujumbe huo. Mathalani, katika 1950 ndugu mmoja Mkorea alikamatwa na kuhojiwa. Yeye alifikiri angeuawa lakini aliazimia kutoa ushuhuda kabla hilo halijatukia. Soma juu yake na wengine wanaoishi katika nchi moja ambayo mmoja kati ya kila wahubiri wanne ni painia.
KOSTA RIKA: Christopher Columbus alitafuta-tafuta lakini hakupata njia ya kufikia Bahari Kuu ya Hindi. Badala yake, yeye alipata nchi na kuipa jina Kosta Rika, linalomaanisha “Pwani Yenye Utajiri.” Utajiri halisi wa nchi hiyo ni watu ambao wamepata kuwa waabudu wa Yehova. Katika 1918 Kosta Rika ilikuwa na namba ya nne iliyo kubwa zaidi ya Mashahidi wa Yehova katika ulimwengu. Leo, inapata kilele kipya kimoja baada ya kingine katika watangazaji wa Ufalme.
Masimulizi haya na yawe msaada wa kuimarisha imani yako na kazi yenye bidii katika kueneza evanjeli ya Ufalme.