Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 7/8 kur. 16-20
  • Kosta Rika—Nchi Ndogo, Unamna Mwingi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kosta Rika—Nchi Ndogo, Unamna Mwingi
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mwingine wa Uvumbuzi wa Columbus
  • Nchi ya Unamna Mwingi
  • Kusanyiko Lisilo na Kifani la Watico
  • Kosta Rika Yahitaji Ulimwengu Mpya wa Mungu
  • Matendo ya Mashahidi wa Yehova Katika Nyakati za Kisasa
    1988 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Mawe ya Mviringo na ya Ajabu ya Kosta Rika
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Yucca Usio na Miiba—Mmea Wenye Kubadilika Isivyo Kawaida
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 7/8 kur. 16-20

Kosta Rika—Nchi Ndogo, Unamna Mwingi

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA KOSTA RIKA

KWAMBA Kosta Rika ni nchi ndogo inakuwa dhahiri muda mfupi urukapo kwenye Uwanja wa Ndege wa San José, kilometa chache nje ya jiji kuu. Dakika moja mwaruka juu ya Bahari ya Karibea, na dakika baadaye mwaruka chini-chini juu ya Pasifiki, mkijitayarisha kutua. Kosta Rika, nchi ya wakazi wapatao milioni tatu, ni ukanda mwembamba wa halinchi ya milima-milima na volkeno ulio katikati ya Nikaragua na Panama. Ni mojapo ya mataifa saba ambayo hufanyiza Amerika ya Kati, kutia ndani ile Isthmus ya Panama, ule muungo wa nchi kati ya Mexico katika Amerika Kaskazini na Kolumbia katika Amerika Kusini.—Ona ramani, ukurasa 17.

Mara unapofahamu ulipo, unavutiwa na vuvumuko la majani, urembo wa kijani kibichi wa mashambani. Yaonekana kwamba kila upande uangaliao, unaona miti ya mvumo, migomba, na miwa pamoja na mashamba ya kahawa na aina nyingi za mimea ya kuingizwa kutoka nje, vichaka, na maua. Kosta Rika ni paradiso ya wanabotania. Lakini kabla ya kufyonzwa na nchi hii yenye kuvutia, acheni tuone historia yayo kidogo.

Mwingine wa Uvumbuzi wa Columbus

Katika 1502, Christopher Columbus, katika safari yake ya nne, alipatwa na dhoruba akiwa pamoja na msafara wake kwenye bahari ya ile ijulikanayo sasa kuwa Honduras. Akitafuta mahali pa kujisitiri, aliabiri sehemu ya Nikaragua iitwayo sasa Mosquito Coast naye akatia nanga kwenye kijiji kidogo chenyeji kiitwacho Cariari. Alivutiwa na uchangamfu wa hao watu pamoja na ule uoto wenye kusitawi sana. Hata alivutiwa na mapambo ya dhahabu ambayo baadhi ya wenyeji walivaa. Columbus, katika uchu wake wa dhahabu, alidhania tu kwamba hii ingekuwa pwani yenye utajiri wa madini yenye thamani. Kama ilivyothibitika baadaye, matumaini yake yaliambulia patupu, baada tu ya mvinjari Mhispania kuiita hiyo nchi Kosta Rika, ama Pwani yenye Utajiri.

Katika mkondo wa historia, Kosta Rika ilijikwanyua kutoka Uhispania na kupata uhuru wayo. Katika 1949, baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya muda, hiyo nchi ikawa isiyo na kifani katika historia ya kisasa—rais mshikilizi, José Figueres, alirasimu katiba ambayo ilivunjilia mbali jeshi! Hatua hii kubwa iliwahimiza baadhi ya washiriki wa dhehebu la American Quakers kuhamia Kosta Rika, ambapo walianzisha kiwanda cha jibini, katika Santa Elena. Ikiwa miongoni mwa baadhi ya nchi zenye misukosuko za Amerika Kusini, Kosta Rika kwa kweli imekuwa kitivo cha amani.

Nchi ya Unamna Mwingi

Tukisafiri kupitia eneo dogo la nchi ili kuzuru volkeno za Poás na Arenal, tulivutiwa na unamna mwingi wa mimea na miti, yale maua ya kitropiki, bustani za maua machanga zilizopaliliwa na kuzingwa na nyavu nyeusi, na ulimaji wenye utokezaji mwingi wa stroberi. Tulijihisi wadogo kando ya majani makubwa ya mmea wa sombrilla del pobre (mwavuli wa mtu maskini). Sehemu za miinamo ya vilima zilifunikwa na kijani kibichi kizito cha mimbuni iliyoshehenezwa na beri zayo zilizo nyekundu.

Katika Kosta Rika, vipepeo viko kila mahali. Mnamo mfikio wa San José, kuna mashamba kadhaa ya kufuga vipepeo ambayo katika hayo unaweza kuona na kupiga picha vipepeo katika mazingira yavyo ya asili. Kitabu kimoja cha mwongozo chasema kwamba “kuna vipepeo wengi katika nchi hii ndogo kuliko walioko katika Marekani yote.” Pia chataarifu kwamba “wanasayansi sasa wanajua kwamba Kosta Rika ni moja ya maeneo yenye unamna mwingi wa kibiolojia ulimwenguni.” Si ajabu kwamba wanabotania na wanabiolojia humiminika kuchunguza unamna wa uhai katika nchi ndogo ya Kosta Rika—Ona sanduku lililoambatanishwa.

Kielelezo kingine cha unamna katika mazingira ya asili ni ndege wa Kosta Rika. Unahitaji kuwa macho ili kuona baadhi ya hao ndege na hata kuwa mwenye kasi mno kuweza kupiga picha yao! Makundi ya parakiti wa kijani-kibichi hufanyiza miingio na miondoko yenye makelele mahali popote waendapo. Wenye kuruka juu walikuwa zopilotes, ama tumbusi weusi, wakitafuta kwa macho makali mlo wao utakaofuata. Katika kivuli cha msitu, huenda upate mwono wa tokani wenye sura mbaya, wenye midomo mikubwa. Tuliona chiriku wa paja manjano na kiskadii mshika-nzi mwenye kifua cha manjano akiruka kupitia miti. Pia tulipata mwono wa msafara ulioruka wa ndegewavumi wakiruka-ruka juu kwenye maua yaliyokuwa karibu kwa ajili ya mwonjo wao ufuatao wa nekta. Kwenye ZooAve (Hifadhi ya Ndege), tulifurahia kuona kila aina ya ndege wa Kosta Rika. Kulikuwa na rukosi makosi, wenye rangi nyingi wakivuta uangalifu wa watu kwa madaha yao. Ala, ndege wengine wengi walilazimika kuwekwa kwenye vizimba, kutia ndani na familia ya bundi wanne, wakiwa wamekaa upande kwa upande, wakionekana kujanjaruka mno.

Kosta Rika ni maarufu kwa unamna wayo mwingi wa mbuga za kitaifa na kibinafsi, hifadhi za Kihindi, na kambi za wanyama-pori. Kwa hakika, karibu asilimia 27 ya ardhi imehifadhiwa, ulinganifu ulio mkubwa zaidi kuliko nchi nyingineo ulimwenguni. Hivyo ikiwa una nia ya kusafiri, unaweza kufanya uchaguzi wa halinchi na mandhari za kimazingira.

Ukienda Kosta Rika, kuna tahadhari moja ndogo ambayo wahitaji kufahamu. Ukiendesha gari huko, huenda ukawiwa radhi kwa kufikiri kwamba madereva wengi walio mbele yako wamelewa. Kwani? Kwa sababu mara kwa mara wao watakata kona na kubeta bila tahadhari. Wao wanafanya nini? Wao wanakwepa mashimo makubwa ambayo yamefika mfumo wa barabara za nchi. Hivyo basi, broshua moja ya watalii ilitaarifu kuhusu hifadhi maarufu ya Monteverde Cloud Forest Reserve hivi: “[Hiyo] yaweza kufikilika tu kupitia kuvumilia saa kadhaa za hali yenye kusikitisha ya barabara; ziara ya siku kadhaa yapendekezwa badala ya kuingia na kutoka haraka katika hifadhi.” Bila shaka, ukisafiri kwa gari lenye mfumo wa kufyonza msukosuko ulio mzuri na magurudumu yenye nguvu, huenda usiathiriwe sana na mashimo haya.

Kwa kweli, kuna mengi sana ya kuona na kujifunza katika Kosta Rika ambayo likizo ya majuma mawili itakuruhusu tu kuonja urembo na unamna wa nchi hiyo yenye kuvutia. Hoteli moja ilikuwa na mionyesho michache katika hifadhi ndogo ya ndege. Mlinzi kwa fadhili alituruhusu kuingia katika vizimba kuchukua picha ya tokani na lithi oseloti. Unamna pia watumika kwa watu wa Kosta Rika wenye ukarimu.

Kusanyiko Lisilo na Kifani la Watico

Tico ni nini? Hilo ni jina lijulikanalo lililopewa watu wa Kosta Rika. Latokana na desturi ya kutumia kiambishitamati udogo -ico katika lugha ya Kihispania. Kwa kielelezo, chiquitico kwa ajili ya mdogo, bonitico kwa ajili ya murua ama maridadi, na jovencitico kwa ajili ya mchanga. Huko nje kwenye Sarchi mji wa mashambani, wanasanaa wa tico ni maarufu kwa picha za carretas, au kigari cha kukokotwa na ng’ombe. Kila moja ni kazi inayotokeza ya usanii. Watalii hununua hivyo visanamu kwa mamia.

Mwishoni mwa 1994, watico walikuwa na fursa ya kuona jambo fulani la kipekee sana katika nchi yao ya Kikatoliki. Desemba 30 hadi Januari 1, 1995, zilikuwa tarehe za mkusanyiko wa kidini wa Mashahidi wa Yehova uliotukia katika stediamu ya kandanda ya kitaifa katika Sabana Park, San José. Ulitukia chini ya kichwa cha Kibiblia Temor Piadoso (Hofu ya Kimungu), na Mashahidi walitoka kote nchini, huku vikundi vidogo vya wajumbe vikiwasili kutoka nchi nyingine za Amerika ya Kati na ya Kusini. Kosta Rika ina Mashahidi watendao zaidi ya 15,000. Hudhurio lingekuwa nini kwenye pindi hii ya kipekee? Ijumaa watu 21,726 walikuja—wachanga, wazee, wazazi, watoto, wote walivalia kinadhifu na kwa kiasi. Jumamosi umati uliongezeka hadi 25,539, na 681 walibatizwa katika vidimbwi vitatu vikubwa vilivyowekwa kwenye pembe moja ya huo uwanja. Jumapili idadi ya wahudhuriaji iliongezeka hadi 27,149! Ulikuwa msisimuko ulioje kwa wamishonari, mapainia (waeneza-evanjeli wa wakati wote), na wanaume, wanawake, na watoto wanyenyekevu wafanyao kazi kwa bidii ili kueneza eneo la Kosta Rika nyumba kwa nyumba. Na jinsi ilivyotia moyo kuona familia nyingi katika stediamu iliyo wazi, zikijisitiri jua chini ya myavuli yenye rangi nyingi!

Programu ilipoisha, maelfu yalitoa vitambaa vyao vya mkono na kupungiana kwaheri. Ilikuwa pindi yenye kugusa moyo.

Kosta Rika Yahitaji Ulimwengu Mpya wa Mungu

Hata ingawa kuna mengi katika nchi hii ya kumkumbusha mmoja kuhusu paradiso—unamna wayo wa mimea na wanyama na tabia-anga yayo—watico, kama watu wa nchi nyingineo yoyote, wanahitaji ile ‘mbingu mpya na nchi mpya’ ambayo Yehova aliahidi kupitia kwa Yesu Kristo. (Isaya 65:17; 2 Petro 3:13; Ufunuo 21:1-4) Hata kama inavyoonekana ulimwenguni pote, pia katika Kosta Rika kuna dalili za umaskini, familia zikiishi katika nyumba zisizotosha. Kisha pia kuna magonjwa na kifo, hali ambazo hufika jamii zote za kibinadamu. Hivyo basi, Mashahidi wa Yehova wanahubiri kwa bidii habari njema ya utawala wa Ufalme wa Mungu, Ufalme ambao Wakristo wote wenye moyo mnyofu huomba katika ile sala maarufu ya Baba Yetu, ama Sala ya Bwana. Chini ya utawala huo mwadilifu ulioahidiwa, unamna mwingi wa Kosta Rika utang’ara kwa wangavu hata zaidi, kwa sifa ya milele ya Mungu.

[Sanduku katika ukurasa wa 19]

Unamna Mwingi Mno wa Kosta Rika

Kile kitabu Costa Rica—A Natural Destination chataarifu hivi: “Kosta Rika ina spishi nyingi mno. Nchi hii ambayo imefunika eneo lipatalo 0.03% la uso wa dunia ni makao ya asilimia 5 ya spishi zote za mimea na wanyama zijulikanazo kuwapo.” Kwa kielelezo kuna:

Kiwango cha chini cha spishi 830 za ndege, kutia ndani tokani na kwezali

Kiwango cha chini cha spishi 35,000 za wadudu

Kiwango cha chini cha spishi 9,000 za mimea aina ya trakiofita

Kiwango cha chini cha spishi 208 za mamalia, kutia ndani oseloti

Kiwango cha chini spishi 220 za reptili, kutia ndani iguanas kubwa

Kiwango cha chini cha spishi 160 za amfibia, kutia ndani vyura mshale-sumu

Kiwango cha chini cha spishi 130 za samaki wa maji matamu

Wanasayansi fulani wanakisia kwamba yawezekana kuna spishi milioni moja katika Kosta Rika.

[Sanduku katika ukurasa wa 19]

Volkeno

Kuna kreta zijulikanazo 112 ambazo huenea kutoka zisizotenda hadi zitendazo. Volkeno yenye kuvutia ya Arenal, ambayo ina urefu wa zaidi ya meta 1,500 ni mojapo ya volkeno zenye kutenda sana ulimwenguni. Ukitaka kuiona, ni bora kuchunguza utabiri wa hewa kabla ya kufunga safari ngumu, ya barabara yenye mashimo. Arenal mara nyingi huwa imefunikwa na mawingu.

Volkeno ya Irazú ina urefu wa zaidi ya meta 3,400. Ilikuwa tendaji kutoka 1963 hadi 1965.

Volkeno ya Poás, yenye urefu wa zaidi ya meta 2,700, ni mlima wenye macho mawili—moja jeupe na linalochemka katika kreta yenye kutenda na lile jingine, ziwa la samawati lililozingwa na majani yaliyositawi mno.

[Ramani katika ukurasa wa 17]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

NICARAGUA

COSTA RICA

Arenal

Monteverde

Poás

Sarchi

San José

Cartago

Limón

PANAMA

[Picha katika ukurasa wa 16, 17]

Ukurasa wa 16:

Tokani na Volkeno ya Arenal

Ukurasa wa 17:

1. Kreta ya volkeno ya Poás

2. Makau

3. Dansi ya kitamaduni

4. Bromeliad

5. Mmea wa mwavuli

6. Iquanas

7. Oseloti

[Picha katika ukurasa wa 18]

“Hofu ya Kimungu” Mkusanyiko katika San José; 681 walibatizwa, kutia ndani Digna (mbali kulia)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki