Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb15 uku. 164-uku. 165
  • Aliyepinga Kuwapo kwa Mungu Awa Mtumishi wa Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aliyepinga Kuwapo kwa Mungu Awa Mtumishi wa Mungu
  • 2015 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Habari Zinazolingana
  • Utamwambia Nini Mtu Asiyeamini Mungu?
    Huduma Yetu ya Ufalme—1999
  • Yehova Amefungua Mioyo ya Watu Wengi
    2015 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
  • Je, Inawezekana Kuamini Kuna Muumba?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • “Nililelewa na Wazazi Walioamini Hakuna Mungu”
    Amkeni!—2010
Pata Habari Zaidi
2015 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
yb15 uku. 164-uku. 165

JAMHURI YA DOMINIKA

Mpiganaji Asiyemwamini Mungu Awa Mtumishi wa Mungu

Juan Crispín

  • ALIZALIWA 1944

  • ALIBATIZWA 1964

  • HISTORIA FUPI Zamani hakuamini kuwapo kwa Mungu, sasa amemtumikia Yehova kwa uaminifu kwa miaka 50.

Picha katika ukurasa wa 164

NILIPOKUWA kijana, nilikasirishwa sana na chuki ya kidini. Pia, sikuelewa kwa nini Mungu hakukomesha umaskini na ukosefu wa haki, au kwa nini wanadini wengi hawaishi kupatana na mambo ambayo Biblia inasema. Kwa hiyo, nikaanza kuamini hakuna Mungu, nikidhani kwamba mapinduzi ya kisiasa tu ndiyo yangeubadili ulimwengu.

Mnamo 1962, nilianza kusoma gazeti la Amkeni! Kisha, mwaka wa 1963, nilikubali kufundishwa Biblia na Mashahidi wa Yehova. Mambo niliyojifunza yalibadili kabisa mtazamo wangu. Nilielewa kwamba Mungu si wa kulaumiwa kwa sababu ya mauaji yaliyofanywa na vikundi vya kidini na kwamba Mungu ana kusudi zuri kwa wanadamu. Miezi miwili baada ya kuanza kujifunza, nilianza kuwaeleza wengine kwamba Ufalme wa Mungu utaondoa mfumo huu mwovu wa mambo. Nilibatizwa mwaka wa 1964 na kuwekwa rasmi kuwa painia wa pekee mwaka wa 1966. Naamini kwamba kweli iliokoa maisha yangu, kwa sababu vijana wengi wapiganaji nilioshirikiana nao waliuawa kikatili, walifungwa, au kulazimika kuikimbia nchi. Namshukuru Yehova kwa kunigeuza ili nimwamini, kwani nilikosa tumaini lakini sasa namtumikia Mungu ambaye anaahidi kuleta ulimwengu mpya wenye uadilifu.

Picha katika ukurasa wa 165

Ndugu Crispín akiongoza ibada ya asubuhi Betheli

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki