Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mrt makala 88
  • Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Vita?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Vita?
  • Habari Zaidi
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nani Atakayewaokoa Raia?​—Biblia Inasema Nini?
    Habari Zaidi
  • Vita Nchini Ukrainia Vyaingia Mwaka wa Pili—Biblia Inatoa Tumaini Gani?
    Habari Zaidi
  • 2023: Mwaka Uliojaa Msukosuko—Biblia Inasema Nini?
    Habari Zaidi
  • Vita Vitakwisha Lini?​—Biblia Inasema Nini?
    Habari Zaidi
Pata Habari Zaidi
Habari Zaidi
mrt makala 88
Mwanamume akisukuma baiskeli katika mtaa uliojaa vifusi na magari ya vita yaliyoharibika.

Chris McGrath/Getty Images

KAMPENI YA PEKEE

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Vita?

Ulimwengu unaendelea kuathiriwa na vita vinavyosababisha maumivu na kuteseka kwingi. Ona ripoti zifuatazo:

  • “Tarakimu mpya zinaonyesha kwamba idadi ya watu waliokufa kutokana na vita imeongezeka kuliko miaka 28 iliyopita, hasa kwa sababu ya vita vinavyoendelea nchini Ethiopia na pia Ukrainia.”​—Taasisi ya Utafiti Kuhusu Amani ya Oslo, Juni 7, 2023.

  • “Vita nchini Ukrainia ni moja tu kati ya vita vilivyoongezeka katika mwaka wa 2022. Kwa ujumla, mwaka uliopita jeuri inayosababishwa na mambo ya kisiasa iliongezeka kwa asilimia 27 ulimwenguni pote. Inakadiriwa kwamba watu bilioni 1.7 waliathiriwa na madhara ya vita.”​—The Armed Conflict Location & Event Data Project (ACLED), Februari 8, 2023.

Biblia inatupatia tumaini. Inasema kwamba “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa kamwe.” (Danieli 2:44) Ufalme, au serikali hiyo itakapotawala, Mungu ‘atakomesha vita katika dunia yote.’​—Zaburi 46:9

Ufalme wa Mungu Ni Nini?

Gazeti la “Mnara wa Mlinzi” lenye kichwa “Ufalme wa Mungu Ni Nini?”

Katika mwezi wa Septemba 2023, Mashahidi wa Yehova walishiriki kampeni ya ulimwenguni pote ya kuwafahamisha watu Biblia inasema nini kuhusu habari hiyo muhimu. Tunakualika usome toleo la gazeti Mnara wa Mlinzi lenye kichwa “Ufalme wa Mungu Ni Nini?” Pata majibu ya maswali kama vile:

  • Mfalme wa Ufalme wa Mungu Ni Nani?

  • Ufalme wa Mungu Utaanza Kutawala Dunia Lini?

  • Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki