Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mrt makala 117
  • Jeuri ya Kisiasa—Biblia Inasema Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jeuri ya Kisiasa—Biblia Inasema Nini?
  • Habari Zaidi
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ilitabiriwa watu watagawanyika kwa sababu za kisiasa
  • Mwisho wa jeuri ya kisiasa
  • Amani Duniani—Itapatikanaje?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Jeuri
    Amkeni!—2015
  • Mwisho Wenye Kudumu wa Jeuri—Utakujaje?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Maoni ya Mungu Ni Nini Kuhusu Jeuri?
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Habari Zaidi
mrt makala 117
Bunduki kubwa yenye matundu mawili.

Rui Almeida Fotografia/Moment via Getty Images

ENDELEA KUKESHA!

Jeuri ya Kisiasa—⁠Biblia Inasema Nini?

Kuna visa vingi sana vya jeuri ya kisiasa ulimwenguni.

  •  Nchini Mexico, wanasiasa 39 wameuawa. Idadi hiyo ni kubwa kuliko wakati mwingine wowote. Matukio hayo pamoja na aina nyingine za jeuri ya kisiasa zimewashtua na kuwakengeusha watu kutoka kwa uchaguzi wa mwaka 2023-2024.

  •  Hivi karibuni barani Ulaya, kumekuwa na matukio mengi ya jeuri ya kisiasa kutia ndani jaribio la kumuua waziri mkuu wa Slovakia lililofanywa Mei 15, 2024.

  •  Watu nchini Marekani wameshtuliwa na jaribio la kumuua rais wa awali wa nchi hiyo Donald Trump lililotukia Julai 13, 2024.

Kwa nini kuna jeuri nyingi hivyo ya kisiasa? Je, itakwisha? Biblia inasema nini?

Ilitabiriwa watu watagawanyika kwa sababu za kisiasa

Biblia ilitabiri kwamba katika siku zetu, zinazorejelewa kuwa “siku za mwisho,” watu wengi wangekuwa na mitazamo inayosababisha jeuri na kutoelewana.

  •  “Katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo. Kwa maana watu watakuwa . . . wasio na shukrani, wasio washikamanifu, . . . wasiotaka makubaliano yoyote, . . . wakali, . . . wasaliti, wenye vichwa vigumu, waliojaa kiburi.”​—2 Timotheo 3:1-4.

Pia, Biblia ilitabiri kwamba katika siku zetu lingekuwa jambo la kawaida kwa misukosuko ya kisiasa kutokea na watu kupinga serikali. (Luka 21:9, maelezo ya chini) Hata hivyo, jeuri na mgawanyiko wa kisiasa hautaendelea milele.

Mwisho wa jeuri ya kisiasa

Biblia inaeleza kwamba Mungu ataondoa serikali zote za wanadamu na serikali yake mwenyewe ya mbinguni itachukua mahali pake.

  •  “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao . . . utazipondaponda na kuzikomesha falme hizi [nyingine] zote, nao pekee utasimama milele.”​—Danieli 2:44.

Ufalme wa Mungu utawaunganisha watu kikweli na kuleta amani ulimwenguni pote.

  •  Mtawala wake, Yesu Kristo, anaitwa “Mkuu wa Amani,” naye atahakikisha kwamba kuhusu “amani, hakutakuwa na mwisho.”​—Isaya 9:6, 7.

  •  Hata sasa, raia wa Ufalme huo wanajifunza jinsi ya kuishi kwa amani. Biblia inasema hivi kuwahusu: “Watafua panga zao ziwe majembe ya plau na mikuki yao iwe miundu. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.”​—Isaya 2:3, 4.

Ili ujifunze mengi zaidi, soma makala yenye kichwa “Ufalme wa Mungu Utatimiza Nini?” na utazame video yenye kichwa Ufalme wa Mungu Ni Nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki