Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ijwbq makala 143
  • Je, Kuvuta Sigara Ni Dhambi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kuvuta Sigara Ni Dhambi?
  • Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jibu la Biblia
  • Je, Biblia inasema lolote kuhusu kutumia bangi au dawa nyingine?
  • Sigareti—Je, Wewe Huzikataa?
    Amkeni!—1996
  • Nahitaji Kujua Nini Kuhusu Uvutaji wa Sigara?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Mungu atahisije nikitumia tumbaku?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Mungu ana maoni gani kuhusu Kuhusu Kuvuta Sigara?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Maswali ya Biblia Yajibiwa
ijwbq makala 143
Kuvuta sigara

Je, Kuvuta Sigara Ni Dhambi?

Jibu la Biblia

Biblia haitaji kuvuta sigaraa au njia nyingine za kutumia tumbaku. Hata hivyo, ina kanuni zinazoonyesha kwamba Mungu anashutumu mazoea machafu na yanayodhuru afya, kwa hiyo, anaona kuvuta sigara kuwa dhambi.

  • Kuheshimu uhai. “Mungu . . . huwapa watu wote uhai na pumzi na vitu vyote.” (Matendo 17:24, 25) Kwa kuwa uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu, hatupaswi kufanya jambo lolote linaloweza kufupisha maisha yetu, kama vile kuvuta sigara. Kuvuta sigara ni mojawapo ya sababu kuu za vifo vinavyoweza kuzuiwa ulimwenguni pote.

  • Kupenda jirani. “Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” (Mathayo 22:39) Kuvuta sigara ukiwa karibu na watu wengine kunaonyesha kwamba huwapendi. Watu ambao kwa ukawaida wanapumua moshi kutoka kwa mtu anayevuta sigara, wanaweza kuathiriwa zaidi na magonjwa yaleyale ambayo mara nyingi huwapata wavuta-sigara.

  • Uhitaji wa kuwa mtakatifu. “Mtoe miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, na yenye kukubalika kwa Mungu.” (Waroma 12:1) “Acheni tujisafishe kila unajisi wa mwili na roho, tukiukamilisha utakatifu katika kumwogopa Mungu.” (2 Wakorintho 7:1) Kuvuta sigara si jambo la kiasili na halipatani na kuwa mtakatifu​—yaani, kitu safi na kilichotakata​—kwa sababu watumiaji wa tumbaku huingiza kimakusudi mwilini mwao sumu zinazoweza kuharibu mwili wao.

Je, Biblia inasema lolote kuhusu kutumia bangi au dawa nyingine?

Biblia haitaji bangi au dawa nyingine kama hizo kwa jina. Lakini ina kanuni zinazoonyesha kwamba haifai kutumia vitu kama hivyo vinavyomfanya mtu awe mraibu. Mbali na kanuni zilizotajwa tayari, zifuatazo pia zinahusika:

  • Uhitaji wa kudhibiti uwezo wetu wa kufikiri. “Lazima umpende Yehova Mungu wako . . . kwa akili yako yote.” (Mathayo 22:37, 38) “Tunzeni akili zenu kwa ukamili.” (1 Petro 1:​13) Mtu hawezi kudhibiti akili yake kikamili anapotumia dawa vibaya, na watu wengine hata wamekuwa waraibu. Akili zao hukazia fikira kutafuta na kutumia dawa za kulevya badala ya kukazia fikira mawazo yenye kujenga.​—Wafilipi 4:8.

  • Kutii sheria za serikali. “[Wazitii] serikali na mamlaka.” (Tito 3:1) Katika nchi nyingi, sheria zinakataza kabisa matumizi ya dawa fulani. Ikiwa tunataka kumpendeza Mungu, tunapaswa kutii sheria za serikali.​—Waroma 13:1.

Tumbaku na Afya Yako

Shirika la Afya Ulimwenguni linakadiria kwamba kila mwaka, karibu watu milioni sita hufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na tumbaku, kutia ndani zaidi ya watu 600,000 ambao wameathiriwa na moshi wa wavutaji sigara. Tumbaku huathiri afya ya watu wanaoitumia na ya watu wanaowazunguka kwa njia zifuatazo.

Kansa. Moshi wa tumbaku una kemikali zaidi ya 50 zinazoweza kusababisha kansa. Encyclopædia Britannica inasema kwamba “inaaminika kuwa moshi wa tumbaku ndio kisababishi kikuu cha asilimia 90 ya visa vyote vya kansa ya mapafu.” Moshi wa tumbaku unaweza kusababisha kansa katika viungo vingine kutia ndani kinywa, koromeo, umio, koo, zoloto, ini, kongosho, na kibofu.

Magonjwa ya mfumo wa kupumua. Moshi wa tumbaku huzidisha uwezekano wa kupata magonjwa ya mfumo wa kupumua kama vile nimonia na homa. Watoto ambao hupumua moshi wa wavutaji sigara wanakabili hatari zaidi ya kupatwa na ugonjwa wa pumu, kohozi la kuendelea, na kuwa na mapafu yaliyodumaa na yasiyofanya kazi vizuri.

Ugonjwa wa moyo. Wavuta sigara wanakabili hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kiharusi au ugonjwa wa moyo. Kaboni monoksidi iliyo katika moshi wa tumbaku hupita kwa urahisi kutoka kwenye mapafu kuingia kwenye mfumo wa damu, na kuchukua mahali pa oksijeni. Kwa kuwa kunakuwa na upungufu wa oksijeni katika damu, moyo unalazimika kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kusambaza oksijeni mwilini.

Kudhuru mimba. Wanawake wanaovuta sigara wakiwa wajawazito wanawazidishia watoto wao hatari ya kuzaliwa kabla ya wakati, wakiwa na uzito mdogo, au wakiwa na kasoro fulani kama vile mdomo uliopasuka. Watoto kama hao hupatwa na matatizo ya kupumua au hufa ghafla.

a Kuvuta sigara hapa kunarejelea kupumua moshi wa tumbaku kimakusudi kutoka kwenye sigara, kiko, au mirija. Hata hivyo, kanuni zinazozungumziwa hapa zinahusu kutafuna tumbaku, kutumia ugoro, sigara za kielektroni zilizo na nikotini, na bidhaa nyingine kama hizo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki