18 Mnapaswa kula vitu hivyo mbele za Yehova Mungu wenu mahali ambapo Yehova Mungu wenu atachagua+—ninyi na wana wenu, mabinti wenu, watumishi wenu wa kiume na vijakazi wenu, na Mlawi yeyote aliye ndani ya majiji yenu; nanyi mtashangilia mbele za Yehova Mungu wenu katika kazi zenu zote.