2 Wazao waliobaki wa Manase waligawiwa nchi yao kwa kura kulingana na koo zao, yaani, wana wa Abiezeri,+ wana wa Heleki, wana wa Asrieli, wana wa Shekemu, wana wa Heferi, na wana wa Shemida. Hao ndio wazao wa kiume wa Manase mwana wa Yosefu, kulingana na koo zao.+