19 Basi mfalme akamuuliza: “Je, Yoabu ndiye aliyekuambia ufanye hivi?”+ Mwanamke huyo akajibu: “Kwa hakika kama unavyoishi, Ee bwana wangu mfalme, ni kama tu ulivyosema bwana wangu mfalme, kwa kuwa Yoabu mtumishi wako ndiye aliyeniagiza mimi mtumishi wako na kuniambia niseme maneno hayo yote.