4 Mara tu mfalme aliposikia neno ambalo mtu wa Mungu wa kweli alikuwa amesema dhidi ya madhabahu huko Betheli, Yeroboamu akanyoosha mkono wake kutoka kwenye madhabahu na kusema: “Mkamateni!”+ Mara moja mkono aliokuwa amemnyooshea ukakauka, naye hakuweza kuurudisha nyuma.+