6 Sasa mfalme akamwambia mtu wa Mungu wa kweli: “Tafadhali, niombee kibali kutoka kwa Yehova Mungu wako, na usali kwa ajili yangu ili nirudishiwe mkono wangu.”+ Ndipo yule mtu wa Mungu wa kweli akaomba kibali kutoka kwa Yehova, na mkono wa mfalme ukarudi kama ulivyokuwa mwanzoni.