29 Kwa hiyo Mfalme Yehoramu akarudi Yezreeli+ ili apone majeraha aliyopata kutoka kwa Wasiria huko Rama alipopigana na Mfalme Hazaeli wa Siria.+ Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka kwenda Yezreeli kumwona Yehoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.