23 Lakini Ornani akamwambia Daudi: “Uchukue uwe wako, bwana wangu mfalme fanya lolote unaloona ni jema. Tazama, ninatoa ng’ombe kwa ajili ya dhabihu za kuteketezwa na kifaa cha kupuria+ utakachotumia kama kuni na ngano ya toleo la nafaka. Ninatoa vitu hivi vyote.”