20 Vyombo vyote vya kunywea vya Mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hakukuwa na kitu chochote kilichotengenezwa kwa fedha, kwa maana fedha ilionwa kuwa si kitu katika siku za Sulemani.+