13 Kisha nikawaweka kuhani Shelemia, Sadoki mwandishi, na Pedaya aliyekuwa Mlawi wasimamie maghala, na msaidizi wao alikuwa Hanani mwana wa Zakuri mwana wa Matania, kwa maana walionwa kuwa wanaume wenye kutegemeka. Walikuwa na jukumu la kuwagawia ndugu zao.