6 Basi wakamchukua Yeremia na kumtupa ndani ya tangi la maji la Malkiya mwana wa mfalme, lililokuwa katika Ua wa Walinzi.+ Wakamshusha Yeremia ndani kwa kamba. Basi hapakuwa na maji ndani ya tangi hilo, ila matope tu, naye Yeremia akaanza kuzama ndani ya matope.