40 Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Yehova baada ya Nebuzaradani+ mkuu wa walinzi kumwachilia huru kutoka Rama.+ Alikuwa amempeleka huko akiwa amefungwa pingu mikononi, naye alikuwa miongoni mwa watu wote waliohamishwa kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babiloni.