8 Kwenye mpaka wa Yuda, kuanzia mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi, mchango mtakaoweka kando unapaswa kuwa na upana wa mikono 25,000,+ nao unapaswa kulingana na urefu wa zile sehemu nyingine za makabila kuanzia mpaka wa mashariki hadi mpaka wa magharibi. Patakatifu patakuwa katikati yake.