36 “Wakati huo ufahamu wangu ukanirudia, nami nikarudiwa na utukufu wa ufalme wangu, ukuu wangu, na fahari yangu.+ Maofisa wangu wakuu na watu mashuhuri walinitafuta kwa bidii, nami nikarudishwa kwenye ufalme wangu, na hata nikaongezewa ukuu mwingi zaidi.