5 Mabaharia wakaogopa sana hivi kwamba kila mmoja wao akaanza kumlilia mungu wake amsaidie. Nao wakaanza kutupa baharini vitu vilivyokuwa melini ili kupunguza uzito wa meli.+ Lakini Yona alikuwa ameshuka chini ndani ya meli, ambamo alikuwa amelala na kushikwa na usingizi mzito.