-
Alijifunza Kutokana na Makosa YakeMnara wa Mlinzi—2009 | Januari 1
-
-
Huku akihisi kuwa hana uwezo wa kusaidia, Yona alienda chini kwenye sehemu za ndani kabisa za meli hiyo na kupata mahali pa kulala. Akalala fofofo.b Kapteni alimpata Yona, akamwamsha, na kumsihi amwombe mungu wake, kama kila mtu alivyokuwa akifanya. Wakiwa na hakika kwamba hiyo haikuwa dhoruba ya kawaida, mabaharia walipiga kura ili kuona ni nani aliyekuwa amewaingiza taabani. Haikosi Yona alizidi kuwa na wasiwasi kadiri mtu mmoja baada ya mwingine alivyoondolewa kupitia kura. Baada ya muda ukweli ukaonekana. Yehova alikuwa akielekeza dhoruba, kutia ndani kura yenyewe, imwangukie mtu mmoja—Yona!—Yona 1:5-7.
-
-
Alijifunza Kutokana na Makosa YakeMnara wa Mlinzi—2009 | Januari 1
-
-
b Tafsiri ya Septuajinti inakazia jinsi Yona alivyolala fofofo kwa kusema kwamba alikuwa akikoroma. Hata hivyo, badala ya kuona usingizi wa Yona kuwa ishara ya kutojali, tunapaswa kukumbuka kwamba nyakati fulani watu walioshuka moyo wanapatwa na usingizi. Yesu alipokuwa na uchungu mwingi katika bustani ya Gethsemane, Petro, Yakobo, na Yohana walikuwa “wakisinzia kwa huzuni.”—Luka 22:45.
-