15 Nao wakaufunika uso unaoonekana wa nchi+ yote, nayo nchi ikawa na giza;+ nao wakawa wakila mimea yote ya nchi na matunda yote ya miti ambayo ile mvua ya mawe ilikuwa imeacha;+ wala hakikubaki chochote cha kijani kibichi juu ya miti wala juu ya mimea ya shambani katika nchi yote ya Misri.+