2 Naye atauleta kwa wana wa Haruni, makuhani, naye kuhani atachukua kipimo cha mkono mmoja wa unga huo laini na mafuta yake pamoja na ubani wake wote; naye ataufukiza uwe kumbukumbu+ lake kwenye madhabahu, kama toleo linalotolewa kwa njia ya moto lililo na harufu ya kumtuliza Yehova.