37 Nao wakaliteka, wakalipiga pamoja na mfalme wake na miji yake yote na kila nafsi iliyokuwa ndani yake kwa makali ya upanga. Hakuacha mtu yeyote aokoke, kulingana na yote aliyokuwa amelitendea Egloni. Kwa hiyo akaliangamiza+ pamoja na kila nafsi iliyokuwa ndani yake.