21 Naye ndiye aliyempiga na kumuua yule mwanamume Mmisri aliyekuwa mkubwa isivyo kawaida.+ Ingawa mkononi mwa yule Mmisri kulikuwa na mkuki, bado yeye alishuka kumwendea akiwa na fimbo, akaunyakua ule mkuki kutoka mkononi mwa yule Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe.+