Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • bm uku. 31
  • Ujumbe wa Biblia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ujumbe wa Biblia
  • Biblia—Ina Ujumbe Gani?
Biblia—Ina Ujumbe Gani?
bm uku. 31
Watu wakifurahia utawala wa Ufalme kwenye dunia Paradiso

Ujumbe wa Biblia

  1. Yehova awaumba Adamu na Hawa wakiwa na tumaini la kuishi milele katika Paradiso. Shetani amchongea Mungu na kutilia shaka haki Yake ya kutawala. Adamu na Hawa wajiunga na Shetani katika uasi, wajiletea dhambi na kifo wao wenyewe na wazao wao

  2. Yehova awahukumu waasi hao na kuahidi Mkombozi, au Uzao, ambao utamponda Shetani, na kubatilisha matokeo yote ya uasi na dhambi

  3. Yehova awaahidi Abrahamu na Daudi kwamba watakuwa babu za Uzao, au Masihi, ambaye atatawala akiwa Mfalme milele

  4. Yehova awaongoza kwa roho manabii kutabiri kwamba Masihi ataondoa dhambi na kifo. Pamoja na watawala wenzake, atatawala akiwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu, ambao utamaliza vita, magonjwa, hata kifo

  5. Yehova amtuma Mwana wake duniani na kumtambulisha kuwa Masihi. Yesu ahubiri kuhusu Ufalme wa Mungu na kutoa uhai wake kuwa dhabihu. Kisha Yehova amfufua akiwa kiumbe wa roho

  6. Yehova amtawaza Mwana wake kuwa Mfalme mbinguni, hatua hiyo ikitia alama mwanzo wa siku za mwisho za mfumo huu wa mambo. Yesu awaongoza wafuasi wake duniani wanapohubiri Ufalme wa Mungu duniani pote

  7. Yehova amwagiza Mwana wake aanze kuitawala dunia. Ufalme huo wazivunja-vunja serikali zote mbovu, waleta Paradiso, na kuwasaidia wanadamu waaminifu kufikia ukamilifu. Haki ya Yehova ya kutawala yatetewa, na jina lake latukuzwa milele

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki