-
Yehova Hubariki Jitihada Yenye Bidii Wakati Gani?Mnara wa Mlinzi—2002 | Agosti 1
-
-
Fikiria mfano wa Raheli, mke wa pili wa Yakobo na aliyependwa sana. Raheli alijua vizuri ahadi ya Yehova ya kumbariki Yakobo. Dada yake Lea, mke wa kwanza wa Yakobo, amebarikiwa kuwa na wana wanne huku Raheli abaki tasa. (Mwanzo 29:31-35) Badala ya kujisikitikia, anaendelea kumsihi Yehova katika sala na kutenda kulingana na sala zake. Kama nyanya yake Sara alivyofanya na Hajiri, Raheli amletea Yakobo, Bilha mjakazi wake awe mke wake wa pili ili kama vile alivyosema, “nami nipate uzao kwa yeye.”a Bilha akamzalia Yakobo wana wawili—Dani na Naftali. Raheli atangaza hivi jitihada zake wakati wa kuzaliwa kwa Naftali: “Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda!”
-