-
Anafikiria Kupungukiwa KwetuMnara wa Mlinzi—2009 | Juni 1
-
-
Lakini namna gani ikiwa mtu huyo hangeweza hata kununua ndege hao wawili? “Basi ataleta sehemu ya kumi ya efa [vikombe nane au tisa] ya unga laini kwa ajili ya toleo la dhambi,” Sheria ilisema. (Mstari wa 11) Kwa ajili ya maskini, Yehova alikubali kwamba toleo la dhambi litolewe bila damu.a Katika Israeli, umaskini haukumzuia mtu yeyote asipate baraka ya kupatanishwa au pendeleo la kurudisha amani kati yake na Mungu.
-
-
Anafikiria Kupungukiwa KwetuMnara wa Mlinzi—2009 | Juni 1
-
-
a Uwezo wa kupatanisha wa mnyama aliyetolewa dhabihu ulikuwa katika damu yake, ambayo Mungu aliiona kuwa takatifu. (Mambo ya Walawi 17:11) Je, hilo lilimaanisha kwamba matoleo ya maskini ya unga hayakuwa na thamani? La. Yehova alithamini matoleo kama hayo yaliyotolewa kwa unyenyekevu na hiari. Isitoshe, dhambi za taifa lote—kutia ndani za maskini—zilifunikwa na damu ya wanyama waliotolewa kwa Mungu katika Siku ya Upatanisho ya kila mwaka.—Mambo ya Walawi 16:29, 30.
-