-
‘Utunze Mzabibu Huu’!Mnara wa Mlinzi—2006 | Juni 15
-
-
Ili kuzalisha divai kwa wingi, wakulima Waisraeli waliitunza sana mizabibu yao. Kitabu cha Isaya kinaeleza jinsi ambavyo mtunza-mizabibu Mwisraeli angechimba shamba lililo milimani na kuondoa mawe makubwa kabla ya kupanda “mzabibu bora mwekundu.” Kisha, huenda angejenga ukuta wa mawe, akitumia mawe aliyotoa kwenye udongo. Ukuta huo ungelinda shamba la mizabibu lisikanyagwe na ng’ombe na kuzuia mbweha, nguruwe-mwitu, na wezi. Pia, huenda angechimba shinikizo la divai na kujenga mnara mdogo. Mnara huo ungekuwa mahali penye baridi pa kukaa wakati wa mavuno ambapo mizabibu ilihitaji kulindwa hata zaidi. Baada ya kufanya kazi yote hiyo, angetazamia mavuno mazuri ya zabibu.—Isaya 5:1, 2.a
-
-
‘Utunze Mzabibu Huu’!Mnara wa Mlinzi—2006 | Juni 15
-
-
Isaya aliifananisha “nyumba ya Israeli” na shamba la mzabibu ambalo hatua kwa hatua lilizaa “zabibu-mwitu” au zabibu zilizooza. (Isaya 5:2, 7) Zabibu-mwitu ni ndogo kuliko zabibu za shambani na hazina nyama nyingi, nazo mbegu zake huchukua nafasi kubwa ya tunda. Zabibu-mwitu haziwezi kutumiwa kutengeneza divai wala kuliwa. Huo ni mfano mzuri unaowakilisha taifa lililoasi imani ambalo matunda yake yalikuwa ni uvunjaji wa sheria badala ya uadilifu.
-