Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Wakati wa Nia Njema”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 6. Kinywa cha Mesiya ni kama upanga mkali kwa njia gani, naye amefichwa na kusitiriwa jinsi gani?

      6 Maneno ya Mesiya ya kiunabii yanaendelea kusema: “Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha.” (Isaya 49:2) Wakati ufikapo ili Mesiya wa Yehova aanze huduma yake ya kidunia mwaka wa 29 W.K., kweli maneno na matendo ya Yesu yanakuwa kama silaha kali zilizosuguliwa, zinazoweza kuipenya mioyo ya wasikilizaji. (Luka 4:31, 32) Maneno na matendo yake yanaichokora ghadhabu ya adui mkuu wa Yehova, Shetani, na wawakilishi wake. Kuanzia wakati Yesu anapozaliwa, Shetani anajaribu kumwua, lakini Yesu ni kama mshale uliofichwa katika podo la Yehova mwenyewe.a Anaweza kuutegemea ulinzi wa Baba yake akiwa na uhakika. (Zaburi 91:1; Luka 1:35) Yesu anatoa uhai wake kwa ajili ya wanadamu katika wakati uliowekwa. Lakini wakati utafika ajitokeze akiwa shujaa hodari wa kimbingu mwenye silaha tofauti, upanga mkali unaotoka katika kinywa chake. Safari hii, upanga huo mkali unawakilisha mamlaka ya Yesu ya kutamka hukumu na kuzifikiliza juu ya adui za Yehova.—Ufunuo 1:16.

  • “Wakati wa Nia Njema”
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • “Hakuna shaka kwamba Shetani alitambua kuwa Yesu ndiye Mwana wa Mungu na kwamba ndiye aliyetajwa na unabii kuwa atamponda kichwa (Mwa 3:15), na kwa hiyo alijaribu juu chini kumwangamiza Yesu. Lakini, malaika Gabrieli alipokuwa akimtangazia Maria kuhusu kutungwa mimba ya uhai wa Yesu, alimwambia hivi: ‘Roho takatifu itakuja juu yako, na nguvu ya Aliye Juu Zaidi Sana itakufunika kivuli. Kwa sababu hiyo pia kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.’ (Lu 1:35) Yehova alimlinda Mwana wake. Jitihada za kumwangamiza Yesu akiwa kitoto kichanga hazikufaulu.”—Insight on the Scriptures, Buku la 2, ukurasa wa 868, lililochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki