Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa Kimesiya
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 22 Mesiya alichukua magonjwa ya wengine na kujitwika maumivu yao. Ni kana kwamba aliinua mizigo yao, akaiweka juu ya mabega yake mwenyewe na kuichukua. Na kwa kuwa ugonjwa na maumivu ni matokeo ya hali yenye dhambi ya wanadamu, Mesiya alizichukua dhambi za wengine. Wengi hawakuelewa sababu ya mateso yake na waliamini kwamba Mungu alikuwa akimwadhibu, akimpiga kwa tauni ya ugonjwa wa kuchukiza sana.c

  • Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa Kimesiya
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • c Neno la Kiebrania lililotafsiriwa ‘kupigwa kwa tauni’ linatumiwa pia kuhusu ukoma. (2 Wafalme 15:5) Wasomi fulani wanasema kwamba, wazo ambalo Wayahudi fulani walipata kutokana na Isaya 53:4 ni kwamba Mesiya angekuwa mwenye ukoma. Talmudi ya Kibabiloni hutumia mstari huu kuhusu Mesiya, ikimwita “yule msomi mwenye ukoma.” Tafsiri ya Kikatoliki iitwayo Douay Version, inatoa wazo moja na Vulgate ya Kilatini kwa kuufasiri mstari huo hivi: “Tumemfikiria kana kwamba ni mwenye ukoma.”

  • Yehova Amkweza Mtumishi Wake wa Kimesiya
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 23. Yesu alijitwikaje mateso ya wengine?

      23 Yesu alijitwikaje mateso ya wengine? Gospeli ya Mathayo inanukuu Isaya 53:4 ikisema hivi: “Watu walimletea watu wengi waliopagawa na roho waovu; naye akafukuza hao roho kwa kusema neno, naye akaponya wote waliokuwa na hali mbaya; ili kupate kutimizwa lile lililosemwa kupitia Isaya nabii, akisema: ‘Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na kuchukua maradhi yetu.’” (Mathayo 8:16, 17) Kwa kuwaponya wale waliomjia wakiwa na maradhi mbalimbali, Yesu alijitwika mateso yao. Na maponyo hayo yalitumia nguvu zake. (Luka 8:43-48) Uwezo wake wa kuponya magonjwa ya aina zote—ya kimwili na ya kiroho—ulithibitisha kwamba alitiwa nguvu za kusafisha watu dhambi.—Mathayo 9:2-8.

      24. (a) Kwa nini ilionekana machoni pa watu wengi ni kama Yesu ‘alipigwa kwa tauni’ na Mungu? (b) Kwa nini Yesu aliteseka na kufa?

      24 Na bado, watu wengi waliona ni kama Yesu ‘alipigwa kwa tauni’ na Mungu. Kwani je, yeye hakuteseka kwa uchochezi wa viongozi waheshimiwa wa kidini?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki