Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Anafunua Mambo Ambayo “Lazima Yatendeke Upesi”
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Juni 15
    • Hata hivyo, namna gani miguu ya hiyo sanamu? Biblia inasema kwamba miguu hiyo ni mchanganyiko wa chuma na udongo. (Soma Danieli 2:41-43.) Maelezo hayo kuhusu miguu yanatimia kipindi kilekile ambacho kichwa cha saba, yaani, Serikali Kuu ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani inapoibuka na kupata umaarufu. Kama vile ambavyo kitu kilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa chuma na udongo kilivyo dhaifu kuliko kitu kilichotengenezwa kwa chuma tu, vivyo hivyo pia Serikali Kuu ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani ni dhaifu kuliko serikali ambayo ilitokana nayo. Hilo lilitukia jinsi gani?

      8, 9. (a) Serikali kuu ya saba ya ulimwengu ilionyesha jinsi gani nguvu kama za chuma? (b) Udongo ulio katika miguu ya ile sanamu unafananisha nini?

      8 Nyakati nyingine, kichwa cha saba cha mnyama huyo kimeonyesha nguvu kama za chuma. Kwa mfano, kilithibitisha kwamba kina nguvu kiliposhinda Vita vya Kwanza vya Ulimwengu. Katika Vita vya Pili vya Ulimwengu, kichwa cha saba kilionyesha pia nguvu kama za chuma.c Hata baada ya vita hivyo, mara kwa mara kichwa cha saba kilionyesha nguvu kama za chuma. Hata hivyo, tangu mwanzoni, chuma hicho kimechanganyika na udongo.

      9 Kwa muda mrefu watumishi wa Yehova wamekuwa wakijitahidi kuelewa kile ambacho miguu ya sanamu hiyo inafananisha. Andiko la Danieli 2:41 linasema kwamba mchanganyiko wa chuma na udongo ni “ufalme,” mmoja, si falme nyingi. Kwa hiyo, udongo unafananisha vitu fulani katika utawala wa Serikali Kuu ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani, ambavyo vinaifanya iwe dhaifu zaidi kuliko Milki ya Roma iliyokuwa na nguvu kama chuma ambacho hakijachanganywa na kitu kingine chochote.

  • Yehova Anafunua Mambo Ambayo “Lazima Yatendeke Upesi”
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Juni 15
    • 11 Je, idadi ya vidole vya miguu vya sanamu hiyo vina maana ya pekee? Fikiria jambo hili: Katika maono mengine, Danieli anataja idadi hususa, kwa mfano, idadi ya pembe zilizo kwenye vichwa vya wanyama mbalimbali. Idadi hizo zina maana. Hata hivyo, anapoeleza kuhusu ile sanamu, Danieli hataji idadi ya vidole vya miguu. Kwa hiyo, inaonekana kwamba idadi hiyo si muhimu sana kama vile ambavyo idadi ya mikono, vidole, miguu, na nyayo za sanamu hiyo si muhimu. Danieli anataja kihususa kwamba vidole vya miguu vingekuwa mchanganyiko wa chuma na udongo. Kutokana na maelezo yake, tunaweza kukata kauli kwamba Serikali Kuu ya Ulimwengu ya Uingereza na Marekani ndiyo itakayokuwa ikitawala wakati ambapo “jiwe” linalofananisha Ufalme wa Mungu litakapoipiga miguu ya sanamu hiyo.—Dan. 2:45.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki