Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Waadilifu Watang’aa kwa Uangavu Kama Jua”
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 15
    • “Ufalme wa mbinguni umekuwa kama mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.

  • “Waadilifu Watang’aa kwa Uangavu Kama Jua”
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 15
    • Mt. 13:24

  • “Waadilifu Watang’aa kwa Uangavu Kama Jua”
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 15
    • 4. (a) Mtu anayetajwa katika mfano huo ni nani? (b) Yesu alianza wakati gani na jinsi gani kupanda mbegu hiyo?

      4 Mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake ni nani? Yesu anajibu swali hilo baadaye anapowaeleza hivi wanafunzi wake: “Mpandaji wa mbegu nzuri ni Mwana wa binadamu.” (Mt. 13:37) Yesu, ambaye ni “Mwana wa binadamu,” alitayarisha shamba katika kipindi cha miaka mitatu na nusu ya huduma yake duniani ili apande mbegu. (Mt. 8:20; 25:31; 26:64) Kisha kuanzia Pentekoste ya mwaka wa 33 W.K. na kuendelea, alianza kupanda mbegu nzuri, yaani, “wana wa ufalme.” Inaonekana kwamba mbegu hiyo ilipandwa wakati Yesu, akiwa mwakilishi wa Yehova, alipoanza kuwamwagia wanafunzi wake roho takatifu, na hivyo akawatia mafuta ili wawe wana wa Mungu.b (Mdo. 2:33) Mbegu hiyo nzuri ilikomaa na kuwa ngano. Kwa hiyo, Yesu alipanda mbegu nzuri ili mwishowe akusanye hesabu kamili ya wale ambao wangekuwa warithi na watawala wenzake katika Ufalme wake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki