Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Saa Yake Ilikuwa Haijaja Bado”
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Septemba 15
    • 17. (a) Yesu anapata ujumbe gani wa dharura anapohubiri Perea? (b) Ni nini kionyeshacho kwamba Yesu anafahamu kusudi la hatua anayopaswa kuchukua na wakati barabara wa matukio?

      17 Ujumbe huo wa dharura unatoka kwa Martha na Maria, dada za Lazaro, wanaoishi Bethania ya Yudea. “Bwana, ona! yule ambaye una shauku naye ni mgonjwa,” aliyetumwa anasema. “Ugonjwa huu hauna kifo kikiwa lengo lao,” anajibu Yesu, “bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kupitia huo.” Ili kutimiza kusudi hilo, Yesu anaendelea kukaa kimakusudi mahali alipo kwa siku mbili. Kisha anawaambia wanafunzi wake: “Twendeni tuingie Yudea tena.” Kwa mshangao wanamjibu: “Rabi, juzijuzi tu Wayudea walikuwa wakitafuta sana kukupiga kwa mawe, na je, wewe unaenda huko tena?” Lakini Yesu anafahamu kwamba ‘saa za nuru ya mchana’ zinazobaki, au muda ambao Mungu ametenga kwa ajili ya huduma yake duniani, ni mfupi. Anajua barabara anachopasa kufanya na kwa nini.—Yohana 11:1-10.

  • “Saa Yake Ilikuwa Haijaja Bado”
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Septemba 15
    • 21. Muujiza wa kufufuliwa kwa Lazaro unakuwa mwanzo wa nini?

      21 Kwa hiyo, kwa kukawia kufika Bethania, Yesu anafanya muujiza ambao hakuna yeyote awezaye kuupuuza. Kwa nguvu kutoka kwa Mungu, Yesu anamfufua mtu ambaye amekuwa mfu kwa siku nne. Hata Sanhedrini iliyo maarufu inalazimika kuutambua muujiza huo na inamhukumia kifo Mfanya-Miujiza huyo! Hivyo, muujiza huo unakuwa mwanzo wa badiliko kubwa katika huduma ya Yesu—badiliko kutoka wakati ambapo “saa yake ilikuwa haijaja bado” hadi wakati ambapo “saa imekuja.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki