-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na yeye alimvurumisha ndani ya abiso na akaifunga na akatia kalafati juu yake, ili asipate kuongoza vibaya mataifa tena mpaka miaka elfu ilipokuwa imekwisha. Baada ya vitu hivi ni lazima yeye aachwe legelege kwa kitambo kidogo.”—Ufunuo 20:1-3, NW.
-
-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Huyu ambaye ni mmezaji, mdanganyaji, mchongezi, na mpinzani mwenye sifa mbaya sana anafungwa mnyororo na kuvurumishwa “ndani ya abiso,” ambayo inashindikwa ndi ndi ndi na kutiwa kalafati kikiki, “ili asipate kuongoza vibaya mataifa tena.” Huku kutiwa kwa Shetani ndani ya abiso ni kwa muda wa miaka elfu moja, wakati huo uvutano wake juu ya aina ya binadamu utakuwa haupo tena kama wa mfungwa aliye ndani ya gereza la shimo lenye kina kirefu. Malaika wa abiso anamwondolea mbali kabisa Shetani asiwe na mgusano wowote na Ufalme wa uadilifu. Lo! ni kitulizo kama nini kwa aina ya binadamu!
-
-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
7. (a) Ni katika hali gani Shetani na roho waovu wake watakuwa wakiwa ndani ya abiso, na sisi twajuaje? (b) Je! Hadesi na abiso ni kitu kile kile? (Ona kielezi cha chini.)
7 Je! Shetani na roho waovu wake watakuwa wakitenda wakiwamo ndani ya abiso? Basi, kumbuka hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, mwenye vichwa saba ambaye “alikuwako, lakini hayuko, na bado yu karibu kupanda nje ya abiso.” (Ufunuo 17:8, NW) Alipokuwa katika abiso, ‘alikuwa hayuko.’ Alikuwa hatendi, hajongei, kwa madhumuni na makusudi yote alikuwa amekufa. Hali kadhalika, mtume Paulo akinena juu ya Yesu, alisema: “‘Ni nani atakayeshuka kuingia ndani ya abiso?’ yaani, kumleta juu Kristo kutoka kwa wafu.” (Warumi 10:7, NW) Akiwa katika abiso hiyo, Yesu alikuwa amekufa.a Basi, inapatana na akili kukata shauri kwamba Shetani na roho waovu wake watakuwa katika hali ya kutotenda kama ya kifo kwa muda wa miaka elfu ya kutiwa kwao ndani ya abiso.
-