Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Cyril na Methodius Watafsiri wa Biblia Waliobuni Alfabeti
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
    • LEO, watu zaidi ya milioni 435 ambao huzungumza lugha za jamii ya Waslavonia wanaweza kupata Biblia katika lugha yao ya kienyeji.a Watu milioni 360 kati yao hutumia alfabeti ya Cyril. Hata hivyo, karne 12 zilizopita hakukuwa na lugha iliyoandikwa wala alfabeti katika lahaja za mababu wao wa kale. Watu waliosaidia kurekebisha hali hiyo waliitwa Cyril na Methodius, ambao walikuwa ndugu wa kimwili.

  • Cyril na Methodius Watafsiri wa Biblia Waliobuni Alfabeti
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
    • Alfabeti na Tafsiri ya Biblia Zaanzishwa

      Wakati wa miezi iliyotangulia kuondoka kwao, Cyril alijitayarisha kwa ajili ya kazi hiyo kwa kuwaandikia Waslavonia alfabeti fulani.b Imesemekana kwamba alikuwa makini sana kuhusu matamshi. Kwa hiyo, akitumia herufi za Kigiriki na Kiebrania, alijaribu kutokeza herufi kwa kila sauti katika matamshi ya Kislavonia. Watafiti fulani wanaamini kwamba tayari alikuwa ametumia miaka mingi akifanya matayarisho ya msingi ya alfabeti hiyo. Na bado kuna shaka kuhusu aina ya alfabeti ambayo Cyril alibuni.—Ona sanduku “Ni Alfabeti ya Cyril au ya Glagol?”

  • Cyril na Methodius Watafsiri wa Biblia Waliobuni Alfabeti
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 1
    • [Sanduku katika ukurasa wa 29]

      Ni Alfabeti ya Cyril au ya Glagol?

      Muundo wa alfabeti ambayo Cyril alibuni umezusha mabishano mengi, kwa kuwa wataalamu wa lugha hawana hakika ilikuwa alfabeti gani. Ile inayoitwa alfabeti ya Cyril inategemea sana alfabeti ya Kigiriki, ikiwa na angalau herufi 12 zaidi zilizobuniwa ili kutokeza sauti za Kislavonia ambazo zilikosekana katika lugha ya Kigiriki. Hata hivyo, hati za awali zaidi za Kislavonia hutumia alfabeti tofauti kabisa, inayojulikana kama alfabeti ya Glagol, ambayo wasomi wengi huamini kwamba ndiyo alfabeti iliyobuniwa na Cyril. Yaonekana kama herufi kadhaa za alfabeti hiyo ya Glagol zatokana na Kigiriki au Kiebrania ambacho huandikwa kwa herufi zenye kuunganishwa. Huenda nyingine zatokana na herufi zenye alama za matamshi za enzi za kati, lakini nyingi ni ubuni wa kwanza ambao ni tata. Alfabeti ya Glagol yaonekana kuwa ndiyo ubuni wa kwanza na wa pekee sana. Hata hivyo, alfabeti ya Cyril ndiyo imesitawi na kutokeza herufi za Kirusi, lugha ya Ukrainia, Kiserbia, Kibulgaria, na Kimakedonia, mbali na lugha nyingine 22 za ziada, ambazo baadhi yazo si za Kislavonia.

      [Artwork—Cyrillic and Glagolitic characters]

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki