Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Zile Nyota na Vile Vinara vya Taa

      5. Yesu anaelezaje “zile nyota saba” na “vile vinara vya taa saba”?

      5 Yohana amemwona Yesu akiwa katikati ya vinara vya taa saba vya dhahabu akiwa na nyota saba katika mkono wake wa kulia. (Ufunuo 1:12, 13, 16) Sasa Yesu anaeleza hilo: “Kwa habari ya siri takatifu ya zile nyota saba ambazo wewe uliona juu ya mkono wangu wa kulia, na ya vile vinara vya taa saba vya dhahabu: Zile nyota saba humaanisha malaika wa yale makundi saba, na vile vinara vya taa saba humaanisha makundi saba.”—Ufunuo 1:20, NW.

      6. Ni kitu gani kinachowakilishwa na hizo nyota saba, na ni kwa sababu gani jumbe zilielekezwa hasa kwa hizo?

      6 Zile “nyota” ni “malaika wa yale makundi saba.” Katika Ufunuo, nyakati nyingine nyota hufananisha malaika halisi, lakini haielekei kwamba Yesu angetumia mwandikaji wa kibinadamu awaandikie viumbe wa roho wasioonekana. Kwa hiyo zile “nyota” lazima ziwe wale waangalizi wa kibinadamu, au wazee, katika makundi, wakionwa kuwa wajumbe wa Yesu.b Hizo nyota zinapelekewa jumbe, kwa kuwa hizo zina daraka la kuangalia kundi la Yehova.—Matendo 20:28.

      7. (a) Ni jambo gani linaloonyesha kwamba Yesu anaposema kwa malaika mmoja hilo halimaanishi kwamba kila kundi lina mzee mmoja tu? (b) Ni nani, kwa kweli, wanaowakilishwa na zile nyota saba katika mkono wa kulia wa Yesu?

      7 Kwa kuwa Yesu anasema kwa “malaika” mmoja tu katika kila kundi, je! hilo linamaanisha kwamba kila kundi lina mzee mmoja tu? La. Mapema kama siku ya Paulo, kundi la Efeso lilikuwa na wazee kadhaa, si mmoja tu. (Ufunuo 2:1; Matendo 20:17) Kwa hiyo katika siku ya Yohana, wakati nyota saba zilipopelekewa jumbe zikasomwe kwenye yale makundi (kutia na kundi la Efeso), nyota hizo lazima ziwe zilisimama badala ya wale wote waliotumikia katika mabaraza ya wazee ndani ya kundi lililopakwa mafuta la Yehova. Hali kadhalika, waangalizi leo husomea makundi barua zinazopokewa kutoka Baraza Linaloongoza, ambalo washiriki walo ni waangalizi wapakwa-mafuta wanaotumikia chini ya ukichwa wa Yesu. Mabaraza ya wazee ya kienyeji yapaswa yahakikishe kwamba shauri la Yesu linafuatwa na makundi yao. Bila shaka, shauri linatolewa kwa manufaa ya wale wote wanaoshirikiana na kundi, na si wazee tu.—Ona Ufunuo 2:11a.

      8. Ni jambo gani linaloonyeshwa na wazee kuwa katika mkono wa kulia wa Yesu?

      8 Kwa kuwa Yesu ndiye Kichwa cha kundi, wazee wanasemwa kwa kufaa kuwa wamo katika mkono wake wa kulia, yaani, chini ya udhibiti na mwelekezo wake. (Wakolosai 1:18) Yeye ndiye Mchungaji Mkuu, nao ni wachungaji walio chini yake.—1 Petro 5:2-4.

  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • b Lile neno la Kigiriki agʹge·los (linalotamkwa “anʹge·los”) humaanisha “mjumbe” na vilevile “malaika.” Kwenye Malaki 2:7, kuhani Mlawi anarejezewa kuwa “mjumbe” (Kiebrania, “mal·’akhʹ”).—Ona kielezi cha chini cha New World Translation Reference Bible.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki