-
Kuwatendea Wengine Kama Mungu AnavyotakaIzingatie Siku ya Yehova Maishani
-
-
Waashuru walijulikana kwa sababu ya kupigana kwa ukali na kuwatesa kikatili wafungwa wa vita—baadhi ya wafungwa waliteketezwa au kutolewa ngozi wakiwa hai, na wengine walipofushwa au kukatwa pua, masikio, au vidole. Kitabu kimoja (Gods, Graves, and Scholars) kinasema: “Waninawi walijulikana sana kwa sababu ya kuua, kupora, kuwakandamiza watu, na kuwatesa walio dhaifu; kupitia vita na jeuri ya kila namna.” Tuna maneno yaliyosemwa na mtu aliyeshuhudia (na labda hata kushiriki) jeuri hiyo. Baada ya kusikia ujumbe wa Yona, mfalme wa Ninawi alisema hivi kuhusu watu wake: “Nao wajifunike nguo za magunia, mwanadamu na mnyama wa kufugwa; na wamwite Mungu kwa nguvu na warudi, kila mmoja kutoka katika njia yake mbaya na kutoka katika jeuri iliyokuwa mikononi mwao.”—Yona 3:6-8.b
-
-
Kuwatendea Wengine Kama Mungu AnavyotakaIzingatie Siku ya Yehova Maishani
-
-
b Jiji la Kala (Nimrud) lililojengwa upya na Ashurnasirpal lilikuwa umbali wa kilometa 35 hivi kusini-mashariki ya Ninawi. Jumba la Makumbusho la Uingereza lina mabamba ya kuta kutoka Kala, na maelezo yake yanasema hivi: “Ashurnasirpal alieleza kinaganaga ukatili na unyama wake katika vita. Wafungwa walinyongwa au kutundikwa mitini kwenye kuta za majiji yaliyoshindwa . . . ; vijana wanaume na wanawake walitolewa ngozi wakiwa hai.”—Archaeology of the Bible.
-