Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/8 uku. 32
  • Mwandishi wa Habari Athamini Amkeni!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwandishi wa Habari Athamini Amkeni!
  • Amkeni!—1998
Amkeni!—1998
g98 5/8 uku. 32

Mwandishi wa Habari Athamini Amkeni!

Pendekezo lifuatalo lilichapishwa katika gazeti la habari la High Country News la Oktoba 13, 1997, linalochapishwa katika Paonia, Colorado, Marekani.

“Shirika la Greenpeace [shirika la kimataifa la mazingira] haliendi tena mlango hadi mlango, lakini kikundi kingine kinaendelea na majadiliano yake ya muda mrefu, mara nyingi kikikazia masuala ya kimazingira. Kinagawanya mamilioni [milioni 19 za kila nakala] ya nakala za habari zake kwa karibu lugha 60 [hasa 81], kutia ndani Kipidgin, Kihiligaynon na Kizulu. Toleo la Julai 8 [1997] katika jalada lake liliuliza: ‘Ni Nani Atakayeokoa Wanyama Wetu?,’ likiwa na habari ndani yake iliyosema juu ya ongezeko la kutoweshwa kabisa kwa ‘afya ya viumbe hai wa sayari,’ (watatu kwa muda wa saa moja), na uharibifu wa ikolojia . . . Nakala ya Ago. 22, 1997, ilizungumzia ‘Shida ya Maji: Tatizo la Tufeni Pote,’ na matokeo ya kuongezeka kwa idadi ya watu, uchafuzi na uvutano wa kimataifa kuhusu matumizi ya mito . . . Ingawa habari hiyo yategemea sayansi na inahusisha mambo mengi, umalizio wa nyingi za makala hizi si mawazo yaliyo mengi ya hali za kimazingira. Wanasema kwamba ikiwa wataka kushiriki kurekebisha upya dunia, ‘Basi tafadhali jifunze analotaka Mungu kutoka kwako kwa kujifunza Biblia.’

“Kikundi hicho ni Mashahidi wa Yehova, na kichapo chenyewe ni Amkeni! Ikiwa hawatafika mlangoni pako, wasiliana na I.B.S.A Box 47788, Nairobi, Kenya.”

Hatungeweza kuieleza habari hii vizuri zaidi kuliko tulivyofanya isipokuwa kwa kuongezea, “au andika ukitumia anwani iliyo karibu nawe iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5 wa Amkeni!”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki