-
Latvia2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Baada ya kuolewa na Kārlis Rezevskis, Alexandra na mume wake walihamia nyumba ndogo ya wazazi wa Kārlis. Nyumba hiyo ilikuwa katika msitu karibu na mji wa Tukums, kilomita 68 kutoka Riga, nayo ilifaa sana kwa mikutano katika majira ya baridi kali. Dita Grasberga, ambaye wakati huo alikuwa akiitwa Andrišaka, anakumbuka hivi: “Nilikuwa mtoto familia yetu ilipokuwa ikihudhuria mikutano katika nyumba ya akina Rezevskis. Nilifurahia kwenda Tukums kwa basi na kutembea katikati ya msitu huku kukiwa na theluji. Kisha, tulipofika kwenye nyumba hiyo, mara nyingi tulisikia harufu nzuri ya mchuzi mtamu uliokuwa ukipikwa.”
-
-
Latvia2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Wakati wa kiangazi, akina ndugu walifanya mikutano katika misitu, kando ya maziwa, au kando ya bahari. Kama ilivyo katika nchi nyingine za Sovieti, walitumia sherehe za ndoa na maziko kutoa hotuba za Biblia.
-