Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ni Nani Walio Wahudumu wa Mungu Leo?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Novemba 15
    • 9. Yesu aliwekwa rasmi kuwa mhudumu lini, na nani?

      9 Kwa habari ya ni lini na ni kupitia nani mtu huwekwa rasmi kuwa mhudumu, hebu fikiria kielelezo cha Yesu Kristo. Yeye hakuwa na cheti cha kuwekwa rasmi kuwa mhudumu au digrii kutoka seminari ili kuthibitisha kwamba alikuwa mhudumu, naye hakuwekwa rasmi na mtu yeyote kuwa mhudumu. Basi, kwa nini tunaweza kusema kwamba alikuwa mhudumu? Kwa sababu maneno haya ya Isaya yaliyopuliziwa yalitimizwa kuhusiana naye: “Roho ya Yehova iko juu yangu, kwa sababu alinitia mafuta kutangaza habari njema.” (Luka 4:17-19; Isaya 61:1) Maneno hayo yanatuhakikishia kwamba Yesu aliidhinishwa kutangaza habari njema. Na nani? Kwa kuwa roho ya Yehova ilimtia mafuta kwa ajili ya kazi hiyo, ni wazi kwamba Yesu aliwekwa rasmi kuwa mhudumu na Yehova Mungu. Aliwekwa rasmi lini? Roho ya Yehova ilimjia Yesu alipobatizwa. (Luka 3:21, 22) Kwa hiyo, aliwekwa rasmi kuwa mhudumu wakati wa ubatizo wake.

  • Ni Nani Walio Wahudumu wa Mungu Leo?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Novemba 15
    • 13. Timotheo aliwekwa rasmi lini kuwa mhudumu, na ni kwa nini waweza kusema kwamba maendeleo yake ya kiroho hayakukoma hapo?

      13 Kwa kuzingatia amri ya Yesu kwenye Mathayo 28:19, 20, tunaweza kuwa na hakika kwamba wakati fulani imani ya Timotheo ilimchochea kumwiga Yesu na kubatizwa. (Mathayo 3:15-17; Waebrania 10:5-9) Kwa kufanya hivyo, Timotheo alionyesha ujitoaji wa nafsi yote kwa Mungu. Timotheo alipata kuwa mhudumu alipobatizwa. Tangu wakati huo na kuendelea, uhai wake, nguvu zake na chochote alichokuwa nacho kikawa cha Mungu.

  • Ni Nani Walio Wahudumu wa Mungu Leo?
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Novemba 15
    • 15. Ni nini hutukia mtu anapobatizwa? (Ona kielezi-chini pia.)

      15 Baada ya kusitawisha upendo kwa Yehova Mungu na imani yenye nguvu katika dhabihu ya fidia, mwanafunzi wa Biblia hutamani kujiweka wakfu kabisa kwa Baba yake wa mbinguni. (Yohana 14:1) Yeye hujiweka wakfu kupitia sala ya kibinafsi, kisha anabatizwa kama wonyesho wa hadharani wa kitendo hicho kilichofanywa faraghani. Ubatizo wake ndiyo sherehe ya kuwekwa rasmi kwake kuwa mhudumu kwa sababu wakati huo ndipo anapotambuliwa kuwa mtumishi, di·aʹko·nos, wa Mungu aliyejiweka wakfu kabisa. Ni lazima ajitenge na ulimwengu. (Yohana 17:16; Yakobo 4:4) Amejitoa kabisa kuwa “dhabihu iliyo hai, takatifu, yenye kukubalika kwa Mungu” bila vizuizi wala masharti. (Waroma 12:1)b Yeye ni mhudumu wa Mungu, anayemwiga Kristo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki