Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hicho Kitabu Kiliokokaje?
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
    • c Kitabu Textual Criticism of the Hebrew Bible, cha Emanuel Tov, chataarifu hivi: “Kwa msaada wa uchunguzi wa kaboni 14, 1QIsaa [Hatikunjo ya Isaya ya Bahari Iliyokufa] sasa imepewa tarehe ya kati ya mwaka wa 202 na 107 KWK (tarehe ya uchunguzaji wa maandishi ya kale: 125-100 KWK) . . . Njia iliyotajwa ya kuchunguza maandishi ya kale, iliyoboreshwa katika miaka ya majuzi, na inayoruhusu uwekaji wa tarehe ulio mkamilifu kwa msingi wa kulinganisha umbo na mpangilio wa herufi na vyanzo vya nje kama sarafu na michoro, imejithibitisha kuwa njia yenye kutegemeka kwa kulinganisha.”6

  • Hicho Kitabu Kiliokokaje?
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
    • Miongoni mwazo ni hati ya Maandiko ya Kiebrania iliyovumbuliwa mwaka wa 1947 inayotoa kielelezo cha kadiri ambavyo kunakili Maandiko kulivyokuwa sahihi. Tangu wakati huo hiyo imeitwa “uvumbuzi wa hati ulio mkubwa kupita wote katika nyakati za kisasa.”5

      Alipokuwa akichunga vikundi vyake mapema mwaka huo, mchungaji mchanga Mbeduini alivumbua pango karibu na Bahari Iliyokufa. Ndani yayo alipata mitungi kadhaa ya udongo, mingi yayo ikiwa mitupu. Hata hivyo, katika mmojawapo mitungi hiyo, iliyokuwa imefungwa ndindindi, alipata hatikunjo ya ngozi iliyokuwa imefungwa kwa uangalifu katika kitani na ilikuwa na kitabu kamili cha Isaya cha Biblia. Hatikunjo hiyo yenye kuhifadhiwa vizuri lakini iliyochakaa ilionyesha ishara za kuwa imetengenezwa. Huyo mchungaji mchanga hakutambua hata kidogo kwamba ile hatikunjo ya kale aliyokuwa akishika mikononi mwake hatimaye ingekaziwa uangalifu ulimwenguni pote.

      Ni nini juu ya hati hiyo hasa kilichokuwa cha maana sana? Mwaka wa 1947 hati kamili za Kiebrania za zamani zaidi kupatikana zilikuwa za tarehe ya karibu karne ya kumi W.K. Lakini hatikunjo hii ilikuwa ya tarehe ya kufikia karne ya pili K.W.K.b—muda wa miaka zaidi ya elfu moja mapema.c Wasomi walipendezwa sana kupata matokeo ya kulinganisha hatikunjo hiyo na hati zilizotokezwa baadaye.

      Katika uchunguzi mmoja, wasomi walilinganisha sura ya 53 ya Isaya katika Hatikunjo ya Bahari Iliyokufa na maandishi ya Kimasora yaliyotokezwa miaka elfu moja baadaye. Kitabu A General Introduction to the Bible, chafafanua matokeo ya uchunguzi huo: “Kati ya yale maneno 166 katika Isaya 53, kuna herufi kumi na saba tu zinazotilika shaka. Kumi kati ya herufi hizo zinahusu tu kuendelezwa kwa maneno, ambako hakuathiri maana. Herufi nyingine nne ni mabadiliko madogo katika mtindo, kama viunganishi. Herufi tatu zinazobaki zafanyiza neno ‘nuru,’ ambalo limeongezwa katika mstari wa 11, na haliathiri maana sana. . . . Hivyo, katika sura moja yenye maneno 166, kuna neno moja tu (herufi tatu) linalotilika shaka baada ya miaka elfu moja ya kupitishwa—na neno hilo halibadili sana maana ya hilo fungu.”7

      Profesa Millar Burrows, aliyefanyia kazi hizo hatikunjo kwa miaka kadhaa, akichanganua yaliyomo, alifikia mkataa uo huo: “Tofauti zilizo nyingi kati ya . . . hatikunjo ya Isaya na maandishi ya Kimasora yaweza kufafanuliwa kuwa makosa katika kunakili. Kando na hayo, kwa ujumla kuna mwafaka wenye kutokeza na maandishi yapatikanayo katika hati za enzi ya kati. Mwafaka wa aina hiyo katika hati iliyo ya zamani zaidi sana watoa ushuhuda wenye kuhakikishia wa usahihi wa ujumla wa maandishi ya zamani.”8

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki