Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ripoti ya Ulimwenguni Pote
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Brazili: Miaka miwili iliyopita Renildo alikuwa akiombaomba katika masoko ya mji wao na katika miji jirani. Licha ya kupata marupurupu kwa sababu ya ulemavu, Renildo aliombaomba ili kuongeza mapato hayo. Alichuma pesa nyingi sana kwa kuombaomba hivi kwamba alikuwa na gari na nyumba yenye vitu maridadi. Pia, aliweza kununua vyakula vingi ambavyo kwa kawaida watu wanaoishi katika eneo hilo maskini hawawezi kununua. Alipojifunza Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova alianza kuzingatia mambo ya kiroho maishani, na akafanya uamuzi fulani mzito. Renildo alizungumza na mke wake na watoto wake watatu kuhusu jinsi ambavyo wangeweza kusaidiana kupunguza gharama, halafu akaacha kuombaomba. Muda si mrefu, yeye na watu wa familia yake walifanya maendeleo ya kiroho na wakabatizwa kwenye kusanyiko fulani la wilaya. Sasa Renildo hajulikani tena kama ombaomba, bali kama mhubiri mwenye bidii wa habari njema. Yeye hutumia muda wa saa 40 kwa wastani kila mwezi katika kazi ya kuhubiri.

  • Ripoti ya Ulimwenguni Pote
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 55]

      Renildo pamoja na familia yake, Brazili

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki