Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Guyana
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kusafiri kwa Mashua Zinazoitwa Kingdom Proclaimers

      Zamani, ndugu walisafiri kwa mashua na mitumbwi yoyote iliyopatikana ili kufika kwenye vijiji vilivyokuwa kando-kando ya mito. Baadaye walinunua mashua ambazo waliziita Kingdom Proclaimer 1, Kingdom Proclaimer 2, hadi Kindom Proclaimer 5. (Mashua mbili za kwanza hazitumiki sasa.)

      Frederick McAlman anasema: “Tulikuwa tukisafiri kwa mashua tukifuata mkondo wa maji ili kuhubiri kuanzia ukingo wa mashariki wa Mto Pomeroon hadi kijiji cha Hackney, umbali wa kilometa 11 kutoka mlango wa mto huo. Huko tulilala vizuri nyumbani kwa Dada DeCambra, ambaye wakati huo alikuwa mkunga katika eneo hilo. Asubuhi na mapema siku iliyofuata, tulisafiri hadi mlango wa mto huo kabla ya kuuvuka na kwenda kwenye ukingo wa magharibi. Kisha tulisafiri kwa mashua umbali wa kilometa 34 hadi Charity.” Kwa miaka mitano, ndugu walipiga makasia kwenda upande wa juu na wa chini wa Mto Pomeroon, kabla ya kununua mashua fulani ya zamani iliyokuwa na injini.

      Kwa kawaida haikuwa hatari kusafiri kwenye mito hiyo, lakini ndugu walihitaji kuwa waangalifu kwa kuwa kulikuwa na mashua nyingine kwenye mito. Mashua ya kwanza na ya pili, hazikusafiri kwa kasi kwa kuwa ziliendeshwa kwa kuvuta makasia. Frederick anasema: “Jumamosi moja alasiri, nilipokuwa nikirudi nyumbani baada ya kuhubiri kwenye eneo la Mto Pomeroon, mashua kubwa ya kubeba mizigo iliyokuwa ikisafiri kwa kasi sana iligongana na mashua yangu. Nahodha na wafanyakazi wa mashua hiyo hawakuwa macho kwa sababu walikuwa wamelewa. Nilirushwa kutoka katika mashua yangu Kingdom Proclaimer 1, na kutumbukia mtoni, chini ya mashua yao. Nilizama majini, lakini nikaendelea kupambana ili kujiokoa. Kichwa changu kilikuwa kikigonga sehemu ya chini ya mashua yao, nami nilikuwa sentimeta chache tu kutoka kwenye rafadha yake iliyokuwa ikizunguka kwa nguvu. Kijana mmoja kwenye meli hiyo aliponiona, alijitosa mtoni na kuniokoa. Nilikuwa na maumivu kwa majuma kadhaa kwa sababu ya majeraha, lakini nilishukuru kwamba nilikuwa hai!”

      Frederick hakuvunjwa moyo na mkasa huo. Anaeleza: “Niliazimia kuendelea kuhubiri, kwa sababu watu walioishi kando-kando ya mto huo walipendezwa na Biblia. Katika kijiji cha Sirikie, umbali wa kilometa 11 kutoka Charity, kulikuwa na Funzo la Kitabu la Kutaniko ambalo niliongoza.”

  • Guyana
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 169]

      Kuhubiri kando-kando ya Mto Moruka katika “Kingdom Proclaimer 3”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki