-
Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
FAMILIA YENYE UAMINIFU
Ndugu zetu walikuwa waangalifu sana nyakati zote. Hata hivyo, wengine walipatwa na “wakati na tukio lisilotazamiwa” kwa sababu ya kuwa mahali pasipofaa wakati usiofaa. (Mhu. 9:11) Božo Ðorem, ambaye ni Mserbia, alibatizwa kwenye kusanyiko la kimataifa huko Zagreb mwaka wa 1991. Baada ya kurudi Sarajevo, alifungwa gerezani mara kadhaa, na akiwa huko alitendewa vibaya sana kwa sababu ya msimamo wake wa kutounga mkono upande wowote. Mwaka wa 1994, alifungwa gerezani kwa miezi 14. Tatizo kubwa ni kwamba hangeweza kuwa pamoja na mke wake, Hena, na binti yao mwenye umri wa miaka mitano, Magdalena.
Muda mfupi baada ya Božo kuwekwa huru kutoka gerezani, msiba ulitokea. Alasiri moja yenye utulivu, wote watatu walienda kuongoza funzo la Biblia karibu na nyumba yao. Walipokuwa njiani, utulivu ulivurugwa na mlipuko wa kombora. Hena na Magdalena walikufa papo hapo, na Božo alikufa baadaye hospitalini.
-
-
Nchi Ambazo Zilikuwa Sehemu ya Yugoslavia2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 200]
Familia ya Ðorem, 1991
-