-
Rwanda2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mnamo Mei 2000, Rwanda ikawa ofisi ya tawi, na muda mfupi baadaye, ndugu wakapata uwanja mzuri ambapo wangejenga ofisi ya tawi ili kushughulikia kazi iliyokuwa inaongezeka kwa kasi nchini Rwanda.
-
-
Rwanda2012 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
MATUKIO MUHIMU YA KITHEOKRASI
Kuhusiana na ofisi mpya ya tawi, Ofisi ya Uhandisi ya Kimkoa nchini Afrika Kusini ilichora ramani za ujenzi, na mjenzi fulani wa Rwanda akaajiriwa kufanya kazi hiyo. Wajitoleaji wa kimataifa walisaidia, na Mashahidi wengi wa Rwanda walijitolea kusaidia kutengeneza bustani na kumalizia kazi nyinginezo. Licha ya matatizo fulani-fulani, familia ya Betheli ilihamia jengo hilo maridadi mwezi wa Machi 2006. Baadaye mwaka huo, Guy Pierce wa Baraza Linaloongoza pamoja na mke wake, alikuja kwa ajili ya programu ya pekee ya kuwekwa wakfu kwa jengo hilo mnamo Desemba 2, 2006. Ndugu 553, kutia ndani wajumbe 112 kutoka nchi 15, walihudhuria programu hiyo.
-