-
Habari Njema ya Paradiso TahitiMnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
-
-
Tahiti Yapata Kuwa Ofisi ya Tawi
Kufikia mwaka wa 1974 idadi ya wahubiri wa Ufalme Tahiti ilikuwa imekua kufikia watu 199. Mwaka uliofuata wakati N. H. Knorr na F. W. Franz waliokuwa wakati huo msimamizi na makamu-msimamizi wa Watch Tower Society, walipotembelea Polynesia ya Ufaransa, waliona kwamba lingekuwa jambo lenye kutumika zaidi kuelekeza kazi ya kuhubiri Polynesia ya Ufaransa kutoka Tahiti, si kutoka Fiji kisiwa kilichoko umbali wa kilometa zaidi ya 3,500. Hivyo, Aprili 1, 1975, ofisi ya tawi ya Tahiti ilianzishwa, na mwangalizi wa mzunguko, Alain Jamet, akawekwa rasmi kuwa mwangalizi wa ofisi ya tawi.
-
-
Habari Njema ya Paradiso TahitiMnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
-
-
Kufikia mwaka wa 1983 idadi ya wahubiri ilikuwa imekua hadi watu 538. Mwaka huo jengo kwa ajili ya ofisi ya tawi na Makao ya Betheli lilijengwa Paea.
-