-
Mama Wenye Afya, Watoto Wenye AfyaAmkeni!—2009 | Novemba
-
-
Kupunguza Hatari Wakati wa Kujifungua
“Wakati hatari zaidi kwa mama mja-mzito ni pindi anapopatwa na maumivu ya kuzaa hadi anapojifungua,” anasema Joy Phumaphi, aliyekuwa naibu msimamizi mkuu wa Shirika la Familia na Jamii la WHO. Ni nini kinachoweza kufanywa ili kuzuia matatizo mabaya, kutia ndani yale yanayoweza kuhatarisha uhai, wakati huu muhimu? Kwa kweli, hatua hizo ni rahisi, lakini zinapaswa kuchukuliwa mapema.b Hili ni muhimu hasa kwa watu wanaokataa kutiwa damu mishipani kwa sababu zinazotegemea Biblia au kwa wale wanaotaka kuepuka damu kwa sababu ya hatari zake za kitiba.—Matendo 15:20, 28, 29.
Wagonjwa kama hao wanapaswa kufanya yote wanayoweza kuhakikisha kwamba daktari au mkunga wao ana uwezo na uzoefu wa kutumia matibabu mengine badala ya kuwatia damu mishipani. Pia, huenda ikafaa akina mama waja-wazito wahakikishe kwamba hospitali watakamojifungua iko tayari kushirikiana nao.c Unaweza kumwuliza daktari maswali haya mawili: 1. Utafanya nini ikiwa mama au mtoto anapoteza damu nyingi sana au ikiwa kuna matatizo mengine? 2. Utafanya mipango gani ya badala ikiwa hutakuwa karibu mama anapojifungua?
-
-
Mama Wenye Afya, Watoto Wenye AfyaAmkeni!—2009 | Novemba
-
-
c Wenzi wa ndoa ambao ni Mashahidi wa Yehova wanaweza kuwasiliana na Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali (HLC) ya Mashahidi wa Yehova katika eneo lao kabla ya kujifungua. Washiriki wa halmashauri hiyo hutembelea hospitali na madaktari ili kuwapa habari kuhusu matibabu yasiyohusisha damu ambayo wagonjwa Mashahidi hukubali. Isitoshe, halmashauri hizo zinaweza kusaidia kumpata daktari anayeheshimu imani ya wagonjwa na aliye na uzoefu wa kutibu wagonjwa bila damu.
-